Home > Terms > Swahili (SW) > Mpendwa Abby

Mpendwa Abby

Mpendwa Abby ni jina la sehemu ya ushauri kwenye gazeti iliyoanzishwa mwaka 1956 na Pauline Philips chini ya jina Abigail Van Buren Sehemu hii iliweza kufanikiwa zaidi wakati amabapo wasomaji magazeti walihitaji mambo kuzungumziwa kwa uwazi, ushauri kuhusu ndoa, watoto, kazi na mengi ya mahusiano ya kibinadamu. Mpendwa Abby huchapishwa na zaidi ya magazeti 1,200 na kusomwa na mamilioni ya watu kila siku.

Philips aliibua jina la kalamu la Abigail Van Buren lililofupishwa na kuwa "Mpendwa Abby" kwa kujumlisha jina la mhusika wa Biblia Abigail, mwanamke mwerevu kwente Agano la Kale huku jina la mwisho la Van Buren likitokana na mmoja wa marais wa Marekani aliyempenda sana - Martin Van Buren

Philips aliweza peke yake kuandika sehemu hii ya ushauri hadi kufikia mwaka 2000 ambapo yeye na bintiye Jeanne walianza kutumia pamoja jina lake katika uandishi wa makala haya. Makala sawia na hayo, Muulize Ann Landers, yaliwenza kuandikwa kuanzia mwaka 1955 hadi 2002 na dadake Philip, Eppie Lederer

Pauline Philips, mwandishi wa mwanzo wa makala ya Mpendwa Abby alifariki mnamo Januari 16, 2013 akiwa na umri wa miaka 94 baada ya muda mrefu wa kuugua Alzheimer

0
Collect to Blossary

Member comments

You have to log in to post to discussions.

Terms in the News

Featured Terms

ogongo3
  • 0

    Terms

  • 0

    Blossaries

  • 3

    Followers

Industry/Domain: People Category: Musicians

Perry Band (almasi, Watu, wanamuziki)

Perry Band ni kundi la muziki nchini, linaloundwa na ndugu zake watatu: Kimberly Perry (gitaa, pianist), Reid Perry (bass gitaa), na Neil Perry ...

Contributor

Featured blossaries

Advanced 4

Category: Education   1 1 Terms

Interesting Apple Facts

Category: Business   7 18 Terms